How to Make Yogurt- Swahili

Jinsi ya kutengeneza yogurt (Gorogoro/Mnando)

Ili kutengeneza yoghurt pale nyumbani unahitaji vitu vifuatavyo;

 

 • Maziwa lita tano;
 • Nusu kikombe ya yoghurt iliyonunuliwa dukani
 • Chombo safi cha kuiweka yoghurt utakoyoitengeneza.
 • Friji

 

Jinsi ya kutengeneza

 1. Twaa lita tano ya maziwa yaliyo bora ambayo hayana dawa yoyote au kuongezwa chochote.
 2. Chemsha hayo maziwa hadi yafikishe kiwango cha nyuzi joto cha 85 digri Celcius kwa jiko na uyawache hapo kwa muda wa dakika mbili au chemsha kwa dakika mbili ili uweze kuua viini vyovyote.
 3. Mwaga hayo maziwa kwa chombo kirefu ambacho kimeoshwa na maji moto kisha wacha hayo maziwa yatulie hadi yafikishe kiwango cha nyuzi joto cha 43 digri Celcius.
 4. Chukua nusu kikombe cha yoghurt uliyonunua dukani kisha upashe moto polepole hadi kiwango sawia cha joto kama vile tu ulivyoyachemsha maziwa hapo awali
 5. Changanya maziwa yaliyopashwa moto pamoja na yoghurt nusu kikombe kisha ufunike chombo kabisa
 6. Weka huo mseto wa yoghurt na maziwa mahali ambapo nyuzi joto haibadiliki kama vile kikapu cha kupika (cooking basket), joto liwe la 43 digri Celcius ambayo ni vuguvugu na waweza kushika kwa mkono bila kuchomeka, kisha uyaache kwa muda wa masaa sita.
 7.  Ondoa kifuniko kisha uyaache yapoe kwa muda wa dakika thelathini hadi yatimize nyuzi joto ya chumba
 8. Ongeza fleva ikiwa inahitajika kisha uvuruge pole pole
 9. Pakia kwenye vyombo visafi
 10. Hifathi kwenye friji kwa muda wa masaa kumi hadi kumi na mawili

Yoghurt yako iko tayari kuuzwa .

 

Kumbuka ya kwamba matunda yanaweza kuongezwa kwa yoghurt ili kuifanya iwe na ladha nzuri, bora Zaidi na yenye ubora wa kiafya

 

Print Friendly, PDF & Email
Share

You may also like...

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Share
Share